×

Bavicha Wajilipua, “Hakuna Ajira, Wanachukua Elfu 20” – Video

Baraza la Vijana wa Chadema (BAVICHA) wanazungumza na Umma kupitia waandishi wa habari kuhusu mambo mbalimbali yaliyotokea nchini. Moja ya mambo ambayo BAVICHA wanazungumzia ni pamoja na ukosefu wa ajira na tatizo la mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu.

 

Akizungumza na wanahabari jijini Dar es salaam, Mwenyekiti wa BAVICHA Taifa, John Justine Pambalu amesema wanahakikisha wanawapambania ili Vijana wa Chuo Kikuu cha Dar waliofukuzwa kwa kudai maslahi ya kupatiwa mikopo na na Bodi ya wanafunzi wa Elimu ya juu (HELBS) wanarudishwa chuoni.

 

Pambalu amesema amesikitishwa kwa wanafunzi hao kufukuzwa kwani walikuwa lengo lengo lao ni kupatiwa mikopo na si vinginevyo.

 

Ameeleza kuwa msimamo wa Bavicha ni kuhakikisha wanasimamia Demokrasia nchini katika kupigania haki ya Watanzania na kuomba bunge kupitia upya sheria ili kuondoa sheria ambazo ni kandamizi na kwamba Bavicha wanatafanya mikutano na makongamano nchini kote ili tu Vijana wapate kushiriki demokrasia.

 

Leave a Comment