×

Eti Pombe Zimemzeesha Charlie Adam

UNAMKUMBUKA yule kiungo wa zamani wa Liverpool na Stoke City, Charlie Adam? Jamaa siku hizi yupo zake Reading huko Ligi Daraja la Kwanza England (Championship), lakini juzi wakati akishangilia katika mchezo wa ligi hiyo dhidi ya Fulham, Adam aliibua jambo kwenye mitandao ya kijamii.

 

Adam alifunga bao moja na kuisaidia Reading kushinda 2-1, lakini mashabiki mtandaoni walichukua picha yake akishangilia wakaitupia kwenye mitandao ya kijamii, wakimfananisha na kibabu chenye miaka 74.

 

Mashabiki hao walichukua picha yake wakaiweka sambamba na ya Cristiano Ronaldo, wote wakiwa na miaka 34, huku Adam akiwa anaonekana ni mzee mara mbili zaidi ya Ronaldo. Mashabiki wengi walieleza kuwa jamaa huyo anazeeshwa na unywaji wa pombe nyingi kupita kiasi.

LONDON, England

 

Leave a Comment