×

Ndege ya Ukraine Yaanguka Iran Ikiwa na Abiria 180

NDEGE ya Ukraine iliyokuwa imebeba watu 180  na wafanyakazi wake, imeanguka karibu na mji mkuu wa Iran, Tehran, dakika tatu baada ya kuruka ikitokea katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Khomeini.

 

Video ambayo haijadhibitishwa na iliyowekwa na Shirika la Habari la BBC, inaonyesha ndege hiyo inayaodaiwa kuanguka baada ya kupata tatizo la kiufundi, iliwaka moto angani kabla y kutokea kwa mlipuko mkubwa na kuanguka.

 

 

Hakuna taarifa zozote kuhusu majeruhi au vifo hadi sasa ila video na picha zinazowekwa katika mitandao ya kijamii zinaonesha hakuna mtu yeyote aliyepona.

Timu ya uchunguzi ipo katika eneo la tukio ambapo ndege hiyo PS752 aina ya Boeing 737-800 imeonekana imeanguka baada ya kufikia urefu wa futi 7,925 kutoka usawa wa bahari.

Kuanguka kwa ndege hiyo kunakuja saa kadhaa baada ya Iran kurusha makombora yake kushambulia kambi mbili za jeshi za Marekani zilizopo Iraq ikiwa ni kujibu mapigo ya kuuawa kwa Jenerali Qassem Soleimani.

 

Updates: Kwa mujibu wa Chombo Cha Habari cha Iran, watu wote waliokuwemo ndani ya ndege (Abiria 167 na Wafanyakazi 9) wamefariki katika ajali ya ndege ya Ukraine iliyotokea huko Tehran, Iran.


Ndege hiyo imeanguka dakika tatu baada ya kuruka ikitokea katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Khomeini, ambapo ikiwa angani ilianza kuwaka moto na kisha kulipuka.

 

Leave a Comment