×

Kocha Mpya wa Yanga Atua Dar, Asepa Zenji – Video

Kocha mpya wa Klabu ya Yanga, Luc Eymael raia wa Ubelgiji tayari amewasili jijini Dar es Salaam na kuelekea Zanzibar jioni hii na ataungana na kikosi cha klabu hiyo hiyo kinachoshiriki Michuano ya Kombe la Mapinduzi.

 

Eymael, ametua jijini Dar es Salaam leo Alhamisi, Januari 9, 2019, na ataanza kazi rasmi baada ya kumaliza taratibu za vibali vya kufanya kazi nchini. Leo Saa 2:15 usiku, Yanga itacheza mchezo wa nusu fainali dhidi ya Kombe la Mapinduzi na Timu ya Mtibwa.

 

Akizungumza mara baada ya kutua kwenye ardhi ya Bongo, Eymael amesema kuwa anaona fahari kujiunga na timu kubwa.

 

“Ni furaha yangu kuona kwamba nimepata timu kubwa ndani ya Afrika. Ninaitambua vema falsafa yake na namna ilivyo hivyo nina imani tutakwenda nayo sawa,” amesema Luc.

 

Leave a Comment