
KATIKA hali isiyo ya kawaida, Deus Richard (40), Mkazi wa Kijiji cha Milala Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda mkoani Katavi amempa ujauzito mtoto wake wa kambo aitwaye Monica Shigela (16) ambaye ni mwanafunzi wa darasa la tano, kisha kutoroka naye kwenda kusikojulikana huku akimuacha mke wake pia akiwa na ujauzito.
Deus amemtelekeza mkewe na watoto wadogo watano na kutoweka kusikojulika na mtoto wake huyo aliyempa mimba.
Bi. Mariam Masanja ambaye ndiye mke aliyetelekezwa, amesema kuwa alipobaini uhusiano wa kimapenzi baina ya mwanaye na baba yake aliwaeleza viongozi wa dini, kitendo ambacho kilimkasirisha bwana huyo na kuanza kuonyesha bayana mapenzi yake na mtoto wake.
Aidha, Mariam ameongeza kuwa licha ya ugumu wa maisha anaopitia kwa sasa kutokana na kutelekezwa akiwa na watoto wadogo na pia ndani kukiwa hakuna chakula, anaiomba serikali kumkamata mumewe huyo na kumchukulia hatua kali za kisheria.
Tukio hilo ambalo ni la kushangaza limeaacha simanzi kwa mama huyo na wananchi kwa baba kumpa mimba mtoto wake wa kambo.