×

JK: Nimeitikia Wito wa Rais Magufuli

 

Rais Mstaafu wa awamu ya 4, Jakaya Kikwete hii leo amekamilisha usajili wa laini zake za simu kwa njia za vidole na kushirikisha taarifa hiyo kupitia akaunti yake ya Twitter.

 

Usajili wa laini za simu kwa njia ya vidole unafikia kikomo Januri 20 mwaka huu. Mbali ya kukamilisha usajili huo Kikwete amewahimiza watanzania wengine “kufanya hivyo kwani siku zimebaki chache”.

 

“Nimeitikia wito wa Serikali na Mhe Rais Dkt. John Pombe Magufuli wa kusajili laini za simu kabla ya tarehe 20 Januari, 2020. Nimekamilisha kwa kusajili laini yangu ya mwisho leo. Namshukuru Obrien kutoka Tigo na kunisajili. Nawahimiza na wengine kufanya hivyo kwai siku zimebaki chache.”

 

Leave a Comment