
MCHUNGAJI Japhes Manwa wa Kanisa la Pentekoste Wilayani Kibaha, anatuhumiwa kumchoma moto mikononi na mgongoni mwanaye wa miaka saba ambaye ni mlemavu. Mtoto huyo ni mwanafunzi wa darasa la kwanza katika Shule ya Msingi Kalabaka.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Wankyo Nyigesa, amesema mtoto huyo ni mmoja kati ya watoto wanne wa mchungaji huyo ambapo inadaiwa mchunganyi kafanya hivyo kwa kuwa hampendi mtoto huyo.
Wankyo ametoa wito kwa wazazi kuwaadhibu watoto wao kulingana na umri pamoja na makosa waliyofanya. Pia, ametoa onyo kwa wazazi na walezi wanaotoa adhabu kali ambazo zinaleta madhara kwa watoto.