×

Magufuli Alivyokomesha Fukuza-Fukuza ya Wachimbaji

MGOMBEA urais wa Jamhuri ya Tanzania kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt John  Magufuli, amesema kuwa katika kipindi chake cha uongozi wachimbaji wa wadogo wa madini wamekuwa wakipewa leseni pale wanapogundua maeneo yenye dhahabu badala ya kufukuzwa.

 

Amesema hayo leo Septemba 9, 2020, akiwa anaongea na wananchi wa Geita kwamba tofauti na siku za nyuma,  wachimbaji wadogo wanahesabiwa kama wawekezaji nchini.

 

“Siku za nyuma ilikuwa ukishagundua dhahabu unafukuzwa, wanakuja wakubwa;  tukasema hapana! Wakigundua wanabaki palepale na wanapewa leseni na wao waweze kutajirika kwa sababu tunawahesabu  kama wawekezaji,” alisema Magufuli.

 

Aliendelea, “Tumejitahidi kuwawezesha wachimbaji wadogo kwa kuwatengea maeneo, kufuta ama kupunguza viwango vya kodi walivyokuwa wanalipa na kuwapatia mafunzo na mitambo ya kuendesha shughuli zao za uchimbaji.”

 

Amefafanua kwamba waliweza kuunda sheria zilizoweza kudhibiti utoroshwaji wa madini nchini na kuanzisha soko kubwa mikoani, hivyo kupelekea uuzwaji wa madini kwa wachimbaji wadogo kupanda kutoka kilo 337 hadi kilo 4656.29 kwa mwaka 2019.

 

Leave a Comment