
Maofisa wa afya nchini Ivory Coast wamesema wanahofia kuwa na mgonjwa mwenye virusi vipya vya Corona.
Waziri wa Afya ametangaza kuwa amepata taarifa za Mwanafunzi ambaye jina lake halikutajwa, aliyetokea China, mjini Beijing na kurudi kwao Afrika magharibi siku ya Jumamosi.
Kwa sasa mwanafunzi huyo anafanyiwa vipimo zaidi baada ya kukutwa na mafua makali ambayo ni moja ya dalili za ugonjwa wa Corona.
Imethibitishwa kwamba mgonjwa huyo atakuwa wa kwanza Barani Afrika kufanyiwa vipimo hivyo vya virusi hatari.
Virusi hivyo vilibainika kwa mara ya kwanza katika mji wa China wa Wuhan, na sasa watu 2000 wana virusi hivyo na 56 wamefariki tayari.