
WAZIRI Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa, leo Alhamisi, januari 30, 2020 anajibu maswali ya papo kwa papo kutoka kwa wabunge katika kipindi cha maswali na majibu, Bungeni jijini Dodoma.
Majaliwa amesema wakati Serikali ikiangalia namna ya kuiongezea ufanisi Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) kutoa kwa haraka vitambulisho vya Taifa, amewataka wananchi kutumia namba ya utambulisho kupata huduma zote zinazohitaji kitambulisho cha NIDA.
“Yako maeneo tumeongeza umakini mkubwa…na hasa maeneo ya mipakani…kwa lengo la kuzuia wananchi wa nchi jirani kujipatia kitambulisho cha NIDA nchini Tanzania halafu akafanya mambo yake huku ndani kupitia kitambulisho cha nchi…
“Kila halmashauri ihakikishe wanafunzi wote (wa kidato cha kwanza) wanaenda awamu moja badala awamu mbili kwa sababu hawa wa pili wanakosa baadhi ya mada za kusoma na mitaala haiwezi kwenda pamoja. Kila halmashauri isimamie hilo,” Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa.