
Mwenyekiti wa kamati ya Kudumu ya Bunge ya hesabu za serikali (PAC) amewasilisha taarifa ya kamati hiyo leo bungeni ambapo ndani yake kuna taarifa ya mkaguzi mkuu wa serikali CAG.
Baada ya kuwasilisha taarifa hiyo, wabunge wakapata fursa ya kutoa hoja akiwemo Mbunge wa Iringa mjini, Mchungaji Peter Msigwa, ambaye ameihoji kamati hiyo kwanini haijawasilisha mambo mengine ya msingi ikiwemo masuala ya Floor Meter.