×

Shime: Tutatumia Makosa Ya Uganda Kupata Ushindi

KOCHA mkuu wa timu ya Wanawake wa U20, Bakari Shime amesema kuwa mchezo wao wa marudiano dhidi ya Uganda, utakuwa mgumu lakini watatumia udhaifu wa timu hiyo kupata ushindi.

 

Tanzania inatarajia kushuka dimbani kesho Jumamosi kucheza mchezo wa marudiano dhidi ya Uganda, mchezo wa kutafuta nafasi ya kufuzu kucheza Kombe la Dunia, litakalofanyika nchini India, kati ya mwezi Juni au Julai.

Katika mchezo wa kwanza uliochezwa wiki moja iliyopita katika Uwanja wa Taifa Dar, Tanzania waliibuka na ushindi wa mabao 2-1.

 

Akizungumza na Championi Ijumaa, Shime alisema: “Uganda wanakuwaga imara sana wakiwa katika uwanja wao wa nyumbani, kwa hiyo bila shaka mechi itakuwa ngumu, lakini uzuri ni kwamba kuna madhaifu f’lani ambayo wanayo kwa hiyo sisi tutatumia udhaifu huo kupata ushindi.”

 

Endapo Tanzania watafuzu katika mchezo huu, watakutana na mshindi kati ya Senegal na Siere Leone, ambapo kikosi cha Tanzania kiliondoka jana na wachezaji 19, kuelekea Uganda tayari kwa mchezo huo.

Stori: Issa Liponda, Dar es Salaam

Leave a Comment