×

DC Sabaya: Tunashindwa Kutofautisha Mganga na Mchungaji – Video

Mkuu wa Wilaya ya Hai, Ole Sabaya amewataka viongozi wa dini kabla ya kuwanyooshea vidole viongozi wa kisiasa ni vyema waakanzia kumulika miguuni mwao kama wanatembea katika njia salama na ya kumpendenza Mungu.

 

DC Sabaya ameyasema hayo leo katika Uwanja wa Mashujaa mjini Moshi wakati wa kuagwa kwa miili ya watu 20 waliofariki wakigombania kukanyaga mafuta ya upako ya Mtume Boniface Mwamposa waliofariki juzi Jumamosi, Feb. 1, 2020.

 

“Nawashukuru sana wachungaji na watu wote walizungumza hapa kwa sababu, miongoni mwao hakuna aliyesema ‘Kazi ya Mungu haina makosa, maana yake mmesema kwa hekima na uungwana kwamba kama tungefanya wajibu wetu tungeepusha kuzika watu hawa 20.

 

“Tuifufue kazi ya Mungu katikati ya miaka itusaidie, lakini tusilitumie jina la Mungu mwenye nguvu atishae, kwa ajili ya kujigeuza na kujipatia faida na utajiri kwa ajili ya wanyonge waliosota na kuteswa na shetani.

 

“Ni kweli Wachungaji wananchi wetu wanateseka sana, wana mizigo mizito, wana shida kubwa sana, lakini msigeuze kuwa ni mitaji ya kuwasaidia watu huko mlipo, tendeni kama mnavyopaswa kutendewa na yakitokea haya msikimbie.

 

“Serikali mliotukosoa na kufanya hayo kama wajibu wenu tutafika sehemu tuseme imetosha, kuondoa maisha ya watu kwa ajili ya jina la Mungu, Mganga ananiambia njoo na kuku, mchungaji ananiambia njoo na fruto, utajua nani mganga nani mchungaji?

 

“Tunashukuru viongozi wa dini kwasababu muda mwingi wanatuonya kama serikali, wanatuasa, wanaandika na waraka lakini tunataka mtakapowasha tochi kutazama walioko mbali tunaomba muiwashe kuanzia miguuni mwenu. Tusigeuze shida za watu kuwa mtaji, vifo hivi vitaendelea kuwaumiza watu sana. tusilitumie jina la Mungu kujipatia faida,” amesema Ole Sabaya.

 

 

Leave a Comment