TAHARUKI imeendelea kutikisa katika mitandao ya kijamii na kwa mashabiki wa muziki wa singeli baada ya jana kusambaa kwa taarifa za kifo cha mwanamuziki wa miondoko hiyo, Meja Kunta, anayetamba na kibao chake cha Mamu.
Mapema leo meneja wa Meja, anayeitwa G-Maker, amekanisha taarifa za kifo hicho na kusema kuwa msanii huyo yupo hai na anaendelea na matibabu kufuatia ajali ya gari aliyoipata juzi akiwa njiani kuelekea mkoani Tanga kwenye tamasha la muziki mnene.
