×

Nzige Janga la Kitaifa Somalia

SERIKALI  ya Somalia imetangaza uvamizi wa nzige wa jangwani kuwa janga la kitaifa kwani wadudu hao wamekuwa tishio kubwa kwa usalama wa mazao ya chakula nchini humo.

 

Wataalamu wanasema uvamizi huo wa nzige ambao unayakumba mataifa kadhaa ya Pembe ya  Afrika, unatokana na mabadiliko ya tabianchi, na umetajwa na shirika la kimataifa la chakula na kilimo (FAO) kuwa mbaya zaidi katika kipindi cha miaka 25 iliyopita.

Somalia imesema kwa kuutangaza uvamizi huo kuwa janga la kitaifa, inaazimia kuzidisha juhudi za kupambana na wadudu hao waharibifu.

 

Wizara ya kilimo mjini Mogadishu imesema wadudu hao wanayaweka hatarini maisha ya watu na ya wanyama kwa kula mazao na mimea ya malisho

Leave a Comment