MKUU wa Mkoa wa Kilimanjaro, Anna Mghwira, amesema miili ya watu 20 waliofariki kwenye kongamano la Mtume na Nabii Mwamposa, itaagwa leo Jumatatu, Februari 3, 2020, kwenye Viwanja vya Majengo mjini Moshi na kwamba hadi sasa tayari miili 16 imeshatambuliwa.
Wakati huohuo, Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP) Simon Sirro, amewataka Watanzania kuwa makini kwani kinyume na hapo itakuwa shida sana.
Ameoongeza kuwa iko haja kamati za ulinzi na usalama za wilaya na mkoa kuanza kuyafuatilia makanisa yote nchini na hasa makanisa madogomadogo ambayo sasa yamekuwepo kila mahali.
“Sio kila padri, mchungaji anataka kuwachunga kondoo wake waende kuuona ufalme wa Mungu, wengine wanahangaika na utafutaji tu wa maisha.
“Si kwamba nahukumu lakini kuna mambo ya kujifunza,” amesema.
Iwapo polisi walikuwepo kwenye kongamano hilo la Mwamposa, Sirro amesema ameshatoa maagizo kwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimajaro kufuatilia na iwapo walikuwepo polisi lazima waulizwe imekuwaje hadi watu wakapoteza maisha na wao wakiwepo, kwani sheria lazima ichukue mkondo wake.


