×

Wanafunzi 14 Wafariki kwa Kukanyagana

WANAFUNZI  14 wa shule ya msingi Kakamega nchini Kenya wamefariki baada ya kupata taharuki na kukanyagana shuleni.

 

Mkuu wa kituo cha polisi cha Kakamega,  David Kabena,  amesema kuwa wanafunzi wengine zaidi ya 50 wamejeruhiwa na wapo hospitali kwa matibabu.

Inadaiwa kuwa idadi ya vifo inaweza kuongezeka. Mkanyagano huo ulitokea baada ya kengele ya kumaliza masomo kupigwa na wanafunzi walikuwa wakitoka kuelekea nyumbani.

 

Ripoti zinasema kuwa wanafunzi hao walikuwa wakitoka katika madarasa yao mwendo wa saa kumi na moja jioni wakati mkasa huo ulipotokea. Imedaiwa kwamba baadhi yao walianguka kutoka ghorofa ya tatu ya jengo hilo walipokuwa wakitoka darasani.

Ripoti ambazo hazijathibitishwa zinasema kuwa wanafunzi wawili wapo katika chumba cha dharura katika hospitali iliyopo kaunti ya Kakamega.

Leave a Comment