MWANASIASA wa muungano wa upinzani wa Lamuka nchini Congo DR unaoongozwa na Martin Fayulu, wamevitaka vyombo vya usalama kumwachilia huru mara moja mratibu wa muungano huo, Luc Malembe, anayeshikiliwa hadi sasa na maafisa wa usalama mjini Bunia, katika jimbo la Ituri nchini humo.
Fayulu, ambaye ni mgombea urais aliyeshindwa katika uchaguzi wa urais wa mwezi Desemba 2018 nchini humo, ameendelea kuonyesha upinzani wake dhidi ya utawala wa rais Felix Tshisekedi Tshilombo.
Malembe, alikamatwa Januari 29, kufuatia tuhuma dhidi kuwa alimkashifu Tshisekedi alipohojiwa na vyombo vya habari huko Bunia, alipotakiwa kutoa maoni kuhusu mwaka mmoja wa utawala wa Tshisekedi, kwa mujibu wa mwanasheria wake Rodrigue Kubuya.

