MWANAMUZIKI kutoka kiwanda cha Bongo Fleva, Isabela Mpanda ametoa kali ya mwaka baada ya kusema kuwa mahari yake akiolewa atataka apewe Biblia tu.
Akibonga na Amani, Isabela alisema siku akipata mwanaume wa kumuoa atataka mahari iwe Biblia kwa kuwa ni kitabu kitakatifu ambacho kinadumu milele na mahari hiyo anataka ipokelewe na msanii wa filamu Steven Mengere ‘Steve Nyerere’ kwa kuwa ni kaka yake anayemkubali sana.
“Siku nikipata mume, mahari yangu nataka iwe ni Biblia tu na hiyo mahari ipokelewe na Steve Nyerere maana namkubali sana. Mimi siyo kama wale wanawake wanaojidai eti wanataka mamilioni ndiyo waolewe wakati hakuna hata wanaume wa kuwatolea kiasi hicho cha fedha,” alisema Isabela.