BAADHI ya Watanzania waishio China wameomba kurudishwa nyumbani wakisema tatizo si kukosa nauli ila wamezuiwa kutoka ili kudhibiti #CoronaVirus na kwamba bado hawajaambukizwa virusi hivyo.
“Tumeiona clip. Hii Ni desparate attempt ya vijana kutafuta msaada. Ukweli nii kwamba baadhi wana anxiety, stress, na wengine wanaelekea kwenye depression,” amesema Balozi wa Tanzania nchini China, Balozi Mbelwa Kairuki.
Timu ya wataalamu wa Shirika la Afya Duniani (WHO) imeelekea Beijing nchini China kuchunguza mlipuko wa virusi vya Corona. Hadi sasa virusi hivyo vimesababisha vifo vya zaidi ya watu 1,018 wengine zaidi ya 43,104 wakiambukizwa, huku waliopona ikielezwa wamefikia 4,043.
Aidha, nyota wa filamu za Kichina, Jackie Chan, ametangaza donge nono la Yuan milioni moja (wastani wa milioni 330 za Tanzania) kwa yeyote atakayegundua kinga au tiba dhidi ya virusi vya Corona.
TAZAMA VIDEO HAPA
View this post on Instagram
