×

Madiwani Watano wa Zitto Watimkia CCM – Video

Madiwani watano wa Chama cha ACT Wazalendo kinachoongozwa na Zitto Kabwe, wamejiuzulu nyadhifa zao zote katika chama hicho na kuomba kujiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM) na kupokelewa na Katibu Mkuu wa CCM, Dkt. Bashiru Ally na Katibu Mwenezi, Humphrey Polepole

 

Akizungumza na wanahabari wakati wa kuwapokea wanachama hao wapya, leo Jumatano, februari 12, 2020, Dkt. Bashiru amesema Madiwani hao walikuwa wa Kata za Kasingiriwa, Kagera, Kasimbu, Kipampa na Gungu zote za Manispaa ya Kigoma-Ujiji.

 

 

Madiwani hao Hamduni Nassoro wa Kata ya Kasingiriwa, Ismail Mahmoud wa Kata ya Kagera, Fuad Seif wa Kata ya Kasimbu, Mussa Ngongolwa wa Kata ya Kipampa na Hamisi Rashidi wa Kata ya Gungu wametangaza uamuzi wao huo wa kujiuzulu katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM – Lumumba.

 

Leave a Comment