

Chambega. Uzinduzi huo umefanyika Jana jijini Tanga.

NBC tawi la Tanga Asia Chambega.

BENKI ya Taifa ya Biashara (NBC) imezindua klabu ya biashara mkoa wa Tanga yenye lengo la kuwakutanisha wafanyabiashara wadogowadogo na wakati ili kupeana fursa, mbinu na kujadiliana mambo mbalimbali yanayohusi biashara zao. Aidha benki hiyo imeendesha mafunzo ya kibiashara kwa wafanyabiashara wadogowadogo na wakati kwa lengo pia la kuwaongezea uwezo, uelewa na ubunifu ufanyaji wa biashara zao.
Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa Klabu hiyo ya Biashara mkoani Tanga juzi, Mkurugenzi wa Kitengo cha Biashara NBC, Elvis Ndunguru alisema kuwa benki hiyo imedhamiria kurahisisha huduma za kibenki kwa makundi mbalimbali hususani
wafanyabiashara ambao ni muhimu kwa ukuaji wa uchumi nchini.
Alisema kuzinduliwa kwa klabu hiyo ya Biashara kunafanya klabu za biashara ya benki hiyo kukua nchini huku malengo yake yakiwa ni kuwaunganisha na kuwakutanisha wafanyabishara pamoja ili kutafuta fursa za ufanyaji wa biashara na kubadilishana uzoefu.
Ndunguru alisema klabu hizo za biashara zimekuwa sehemu ya wafanyabiashara kupata masoko na kuongeza kuwa katika kuhakikisha benki inachangia ukuaji wa sekta ya biashara nchini, imeamua kuanzisha vilabu hivyo vya wafanyabiashara (NBC B Clubs) ili kukuza na kuimarisha biashara nchini.
“NMB B Club ni mahali muafaka pa kuelimisha wafanyabiashara juu ya masuala mbalimbali kuhusu biashara na tangu kuanzishwa kwa klabu hizi za biashara, wanachama wamekuwa wakinufaika na mafunzo mbalimbali ikiwemo jinsi ya kutumia vitabu vya mahesabu, elimu ya masoko na pia elimu ya mlipa kodi kwa kushirikiana na mamlaka ya mapato nchini TRA,”
alisema na kuongeza.
“Klabu hizo zimekuwa zikipanua masoko kwa wafanyabiashara, kwa mfano kwa miaka minne mfululizo sasa tumekuwa tukipeleka wafanyabiashara China na mwaka huu tunatarajia kuwapeleka Ujerumani kwa sababu kuna maonesho ya viwanda lakini pia tunafikiria kupeleka watu Ulaya na Marekani kwa ajili ya kukutana na wenye viwanda na wanaotengeneza mashine mbalimbali jambo ambalo litasaidia kukuza uchumi wetu,” alisema.
Alisema mfanyabiashara akiwa mwanachama wa klabu hizo atapata unafuu wa mikopo inayotolewa na benki, anayeweka amana kuweza kupata riba kubwa zaidi na wanaobadilisha fedha za kigeni kupata punguzo gharama za kubadilisha fedha.
Kuhusu mafunzo ya Biashara alisema waliamua kuyatoa baada ya kuona kunauhitaji na umuhimu wa wafanyabiashara kupata uelewa ili kupunguza kupata hasara na kudanganywa na watendaji wasiowaaminifu.
Naye Mkurugenzi wa Jiji la Tanga, Daudi Maheji ambaye alikuwa mgeni rasmi kwenye hafla ya uzinduzi wa klabu hiyo aliipongeza NBC kwa kuamua kufungua klabu na kutoa elimu ya mlipakodi, utunzaji wa kumbukumbu na jinsi ya kuweka mahesabu sawa.
“Niipongeze NBC kwa uzinduzi wa klabu hii na kutoa mafunzo haya kwani moja ya eneo ambalo wafanyabiashara wengi wanakosa ni hili la utunzaji wa taarifa za biashara zao yaania kumbukumbu, hivyo niimani yangu kuwa litapunguza sana migogoro ya wafanyabisha na Serikali hasa TRA wakati wa ukadiriaji wa kodi zao’ alisema Maheji.
Kwa upande wake Ofisa Mkuu Msimamizi wa Kodi kutoka TRA makao makuu, Julius Mjenga alisema wafanyabiashara wanapaswa kuwa makini katika kutunza kumbukumbu za biashara ili kuepusha migororo na TRA hasa wakati wa ukadiliaji wa kodi.
“Napenda kuwaambia wafanyabiashara kwamba ili waweze kukadiliwa kodi zao vizuri ni muhimu watunze kumbukumbu zao, hata hivyo changamoto kubwa inayoonekana kati ya TRA Na wafanyabiashara ni kulalamikia makadirio ya kodi sasa ili hii iondoke watunze kumbukumbu zao,” alisema.
Naye Kaimu Meneja wa Shirika la Kuhudumia Viwanda Vidogo (SIDO) Tanga, Libera Macha alisema wamekuwa wakitoa mikopo kwa wajasiriamali wanaoanza na kuendelea na biashara hivyo watu wasisite kuja kuchukua kwani vigezo ni kuwa na mradi halali unaoendeshwa kwa mujibu wa utaratibu unaotambulika kisheria.
Kwa upande wake mfanyabiashara ambaye ni mteja wa NBC aliyenufaika na klabu za biashara, Haji Mambo alisema kupitia klabu hizo wameweza kuunganishwa na watu mbalimbali duniani ambapo yeye alifanikiwa kwenda China na kuonana na wafanyabiashara
wengine waliombadilisha mawazo na mitazamo katika biashara zake.
Kuhusu National Bank of Commerce (NBC) Benki ya Taifa ya Biashara, NBC ni benki ya zamani kuliko zote nchini Tanzania ikiwa na uzoefu wa zaidi ya miongo mitano. Tunatoa huduma mbalimbali za kibenki kwa wateja wa rejareja, biashara, mashirika na misaada ya uwekezaji, bidhaa na huduma za usimamizi mzuri wa fedha.
Benki hii inaanzia mwaka 1967 ambapo Serikali ya Tanzania ilibinafsisha taasisi zote za fedha, zikiwamo benki. Mwaka 1991, sheria ya mabenki ilirekebishwa na miaka sita baadae, yaan mwaka 1997, taasisi iliyojulikana kama Benki ya Taifa ya biashara, iligawanywa ka;ka tanzu tatu tofau;: NBC Holding Corpora;on, Na;onal Microfiance Bank (NMB) na NBC (1997) Limited. Mwaka 2000, Benki
ya Afrika Kusini, Absa Group Limited, ilipata hisa 55% kutoka NBC (1997) Limited.
Serikali ya Jamuhuri ya Muungano ya Tanzania ilipata 30% ya hisa na Shirika la Fedha la Kimataifa (IFC) kama
mwanachama wa Benki ya dunia (World Bank Group), ilipata 15% ya hisa za benki hii. Taasisi hiyo mpya ikaitwa NBC Limited.
Benki ya NBC ni benki pekee ya kimataifa inayopa;kana ka;ka maeneo mbalimbali nchini. Ikiwa na matawi 5 na mashine za ATM zaidi ya 230, Benki ya NBC inatoa huduma mbalimbali za ukusanyaji fedha za huduma nyingine za kibenki kwa wateja mbalimbali. Benki ya NBC sasa imeajiri wafanyakazi takriban 1,200 nchi nzima. Kwa maelezo zaidi au msaada tupigie +255 76 898 4000/4011 | +255 22 219 3000 | +255 22 551
1000 or email us [email protected]