×

Nyama ya Punda Yazua Balaa

WAZIRI wa Kilimo nchini Uganda, Peter Munya, ameagiza kufungwa kwa machinjio yote ya punda nchini humo na akawataka wamiliki kuchinja wanyama wengine kama vile  ng’ombe na mbuzi.

 

Ametoa maagizo hayo baada ya wakulima kuandamana nje ya ofisi yake wakidai kutokana na kuongezeka kwa mahitaji ya punda, kumeibuka wimbi kubwa la wizi wa wanyama hao.

 

Katika maeneo ya vijini punda  ni sehemu muhimu ya maisha kwani hutegemewa katika kuchota maji, kubeba kuni na shughuli nyingine na ni mwiko kula nyama ya  punda katika jamii zingine.

 

Aidha, kuna hofu kuwa punda nchini humo wanaweza kuisha ikiwa hakuna hatua itakayochukuliwa kuzuia uchinjaji.

 

Inakisiwa punda 1,000 wanachinjwa kila siku na hivyo wanaweza kuisha ndani ya miaka 10 ijayo.

 

Machinjio ya kwanza yalipoanzishwa nchini humo mwaka 2016, punda mkubwa alikuwa akiuzwa kwa USD 50 (Tsh. 115,492) lakini kwa mujibu wa taarifa hivi karibuni bei imefikia USD 200 (Tsh. 461,969).

Leave a Comment