Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Dkt.Anna Mghwira amebaini upotevu wa shilling mil.300 katika ujenzi wa hospital ya wilaya ya siha Mkoani humo.
Anna Mghwira amefika katika hospital hiyo na kuonesha kutorudhishwa na hali ya utekelezaji wa mradi huo ikiwa ni pamoja na kubaini kutomalizika kwa mradi ni kutokana na uhaba wa fedha ambazo serikali ilikwishatoa lakini haijulikani zilipo.
Aidha mkuu wa mkoa huyo ameagiza wote wanaochunguzwa juu ya upotevu huo kurudisha fedha hizo wakati uchunguzii ukiwa unaendelea huku akitaka wote ambao wamehusika waunganishwe katika kesi hiyo na kuwataka kurejesha fedha hizo
Aliyekua mkurugenzi wa halmshauri hiyo amehusishwa pia katika upotevu wa fedha hizo