×

Shamsa Alia Kukosa Bahati ya Kuhongwa

DAR: Mwanamama mkali wa filamu za Kibongo, Shamsa Ford amesema mara nyingi anasikia kuwa mastaa wengi wanahongwa na kuweza kufanya kazi zao, lakini anashangaa yeye bahati hiyo hana.

Shamsa ameliambia Gazeti la IJUMAA WIKIENDA kuwa, anashangaa kusikia wenzake wanahongwa magari na kupangishiwa majumba ya kifahari, lakini kwa upande wake hajawahi kumpata mwanaume wa kumpa anachotaka zaidi ya juhudi zake mwenyewe.

“Mara nyingi watu wanaamini mastaa wanahongwa na hata mimi hilo sikatai, lakini cha kushangaza mimi sijakutana na bahati hiyo.

“Mimi ninapambana mwenyewe tu. Sasa najiuliza, kwa upande wangu kuna nini, mbona wahongaji hawaji kwangu?” Alihoji Shamsa ambaye mwaka jana aliachana na mumewe, Chid Mapenzi.
Stori: IMELDA MTEMA , Wikienda

Leave a Comment