×

Nigeria Yatangaza Kuwepo Mgonjwa Mwenye Coronavirus

WIZARA ya Afya ya Nigeria imetangaza kugundulika kwa mgonjwa wa kwanza wa COVID-19 nchini humo.

 

Waziri wa afya amesema mgonjwa huyo ni raia wa Italia anayefanya kazi jijini Lagos na siku za karibuni alirejea kutoka Milan (Italia) na kwa sasa mgonjwa huyo yuko katika uangalizi wa kimatibabu.

 

Pia wizara hiyo inafanya juhudi kuwatambua watu wote ambao mgonjwa huyo alikutana nao nchini humo.

 

Leave a Comment