×

Azam Yawatema Jaffary Maganga, Idd Cheche

Aliyekuwa kocha msaidizi wa Azam, Idd Nassor Cheche.

UONGOZI wa Azam FC umesema umeachana na msemaji wa timu hiyo,  Jaffary Idd Maganga,  na kocha msaidizi, Idd Nassor Cheche.

 

Taarifa iliyopo ni kwamba wawili hao walipwa “mkono wa kwaheri” jana Machi 2, 2020, wakiwa wamedumu na kikosi hicho kwa muda wa miaka 10.

 

Azam FC kwa sasa ipo chini ya Kocha Mkuu, Arstica Cioaba.

 

Jaffary Idd alianza na timu hiyo wakati ikipambana kupanda daraja huko Dodoma mwaka 2008 wakati huo akiwa ofisa habari wa Mbagala Market na baadaye kujiunga na Azam kama mpiga picha za video wa timu kwa ajili ya kuweka YouTube na kuendelea katika ngazi zingine hadi  sasa.

 

Naye Idd Cheche aliyekuwa mchezaji wa zamani wa timu ya Sigara ya Dar es Salaam, amekuwa na timu hiyo tangu ilipoanza hadi sasa akiwa mmoja watu waliotoa mchango mkubwa katika kuifikisha ilipo sasa, akiipa mataji mawili ; ubingwa wa Kombe la Mapinduzi mwaka 2017 na Kombe la Shirikisho la Azam Sports (ASFC) msimu 2018/2019 akishirikiana na Meja Abdul Mingange.

 

Ameshiriki mafanikio ya timu ya vijana ya timu hiyo (Azam FC U-20), iliyobeba mataji manne, matatu ya Uhai Cup 2008, 2009 na 2012,  na taji la michuano ya vijana ya Rollingstone mwaka 2014.

Leave a Comment