×

Kagere, Luis Waacha Hofu Yanga SC

MSHAMBULIAJI wa Simba, Meddie Kagere na kiungo mshambuliaji, Luis Miquissone, wamemtia kiwewe Kocha Mkuu wa Yanga, Luc Eymael kutokana na kasi yao ya kufunga mabao kwenye ligi.

 

Pacha ya Kagere na Luis imehusika kwenye jumla ya mabao 23 kati ya 52 yaliyofungwa na Simba huku Yanga wakiwa na mabao 27, ambapo Kagere amefunga mabao 14 na kutoa pasi tano za mwisho na Luis akifunga mabao matatu na pasi moja ya bao lililofungwa na Kagere.

 

Akizungumza na Championi Jumatano, Kocha Mkuu wa Yanga, Luc Eymael alisema kuwa ni ngumu kushindana na timu yenye wachezaji wengi wanaofunga mabao jambo analolifanyia kazi kwa umakini ili kupata mbinu itakayompa ushindi.

“Ukweli kwenye mpira huwa haupingiki wachezaji wangu wamefunga mabao machache kuliko wapinzani wangu Simba ila hilo lipo wazi lakini ninachokifanya ni kutafuta mbinu ya kuwapa wachezaji

 

wangu na kuwaondoa hofu ya kumalizia nafasi wanazotengeneza wakiwa ndani ya uwanja, itatusaidia.

 

“Siwezi kuingia kucheza kwa kuwa kazi yangu ni kufundisha, nimewapa maelekezo vijana wangu, nawaamini hawataniangusha katika hili, mashabiki wajitokeze kwa wingi kwani uwepo wao unatupa nguvu,” alisema Eymael.

 

Machi 8, Uwanja wa Taifa, Yanga itawakaribisha Simba ikiwa na kumbukumbu ya kulazimisha sare ya kufungana mabao 2-2 kwenye mchezo wa kwanza uliochezwa Januari 4, 2020.

JIMMY KINDOKI ‘SIMBA Tumewatengenezea Kitandani Waje Kula GOLI TATU’

Leave a Comment