×

Ofisa wa Jeshi Aliyeasi Anyongwa

ALIYEKUWA Ofisa wa ngazi ya juu katika Jeshi la Misri Hisham al-Ashmaw, amenyongwa hii jana baada ya kupewa hukumu hiyo kutokana na kuhusika na mashambulio kadhaa.

 

Taarifa ya kunyongwa kwa al-Ashmawy imetolewa na msemaji wa jeshi la nchi hiyo. Ashmawy aliyekuwa afisa wa kikosi maalumu cha Misri na baadae kuondoka, aliongoza kundi la waasi la Ansar Bayt al-Maqdis lenye makao yake huko Sinai.

 

Kundi hilo baadae lilitangaza kujiunga na kundi linalojiita dola la kiislamu mnamo mwaka 2014. Al-Ashmawy alikamatwa mshariki mwa Libya mwishoni mwa mwaka 2018 na kupelekwa Misri mwezi Mei mwaka uliopita.

 

Kati ya makosa aliyohukumiwa ni pamoja na kupanga shambulio la mwaka 2014 lililosababisha kuuawa wanajeshi 22 wa Misri na pia kuhusika na jaribio la kumuua waziri wa zamani wa mambo ya ndani mnamo mwaka 2013.

 

Leave a Comment