×

Mkutano wa Mbatia Wazuiwa

MKUTANO wa Mwenyekiti wa NCCR Mageuzi Taifa, James Mbatia,  umezuiliwa na ametakia kuripoti kituo kidogo cha polisi Lwangwa wilayani Rungwe.

 

Mbatia ambaye amefika katika jimbo la Busokelo majira ya saa tano asubuhi leo Alhamisi Machi 5, 2020, katika Kijiji cha Kandete alikuwa akisubiriwa na wanachama wa NCCR kwenye mkutano wa ndani.

 

Nje ya ukumbi wa mikutano Mbatia amesema asingezungumza lolote mpaka atakapofika polisi na kujua anaitiwa nini na kuna shida gani.

Leave a Comment