Nabii wa kike nchini Nigeria ambaye anafahamika kwa jina la Patience Akpabio, amewashauri wanawake kutolala na wanaume zao gizani kwa sababu wanazalisha watoto ambao wanakuwa na mitazamo tofauti duniani.
Nabii huyo amezua gumzo mitandaoni nchini Nigeria, baada ya kutoa angalizo hilo katika mtandao wa Facebook, ambapo amewakataza wanawake kufanya mapenzi gizani kwa sababu watoto wanaozalishwa wanakuwa hawana mitazamo chanya na yenye nguvu.






