Makamu wa Rais Samia Suluhu ameitaka jamii kushirikiana na Serikali katika kupambana na ukatili dhidi ya wanawake na watoto ili kufikia malengo ya kutokomeza ukatili huo kwa asilimia 50 ifikapo 2022.
Makamu wa Rais ameyasema hayo kwenye maadhimisho ya siku ya wanawake ambayo yamefanyika kitaifa Mkoani Simiyu yakiwa na kauli mbiu isemayo Kizazi cha Usawa kwa Maendeleo ya Tanzania ya Sasa na Baadaye.