×

Chadema Yalipa Mil. 110 Kuwatoa Mdee, Matiko na Bulaya Gerezani

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimesema kimeanza mchakato wa kuwatoa gerezani Mbunge wa Kawe, Halima Mdee; Esther Matiko (Tarime Mjini) na Ester Bulaya (Bunda).

 

Mkurugenzi wa Itikadi, Uenezi, Mawasiliano na Mambo ya Nje wa Chadema, John Mrema, amesema mpaka sasa wameshalipa faini ya Sh110 milioni iliyotakiwa kulipwa na wabunge hao watatu ili watoke gerezani.

 

Makusanyo ya fedha mpaka leo saa nane mchana:
1. Simu 176,945,600

2.Benki  52,743,400

3. Taslimu 4,000,780

“Jumla tumekusanya 234,469,000. Matumizi sh.40,000,000 Mdee, 30,000,000 Bulaya na 30,000,000 Matiko. Faini zao zimeshalipwa. Asanteni Watanzania,” amesema Mrema.

 

“Tunawashukuru sana Watanzania kwa michango yao wanayoendelea kuchangia, kitendo cha kuchangia kufikisha Mil. 234 ndani ya saa 24 ni jambo kubwa sana. Bado tunahitaji michango zaidi iendelee ili kuweza kuwatoa viongozi wetu wote,” Kaimu Katibu Mkuu wa Chadema, Benson Kigaila.

 

“Kwa njia ya simu tumekusanya Tsh Milioni 176,945,600, Kwa njia benki tumekusanya 52,743,400 na cash tulizopokea hapa makao makuu ni Milioni 4.7, jumla tumepata Milioni 234,” Kaimu Mwenyekiti Chadema, Said Issa Mohammed.

 

“Kutokana na michango ya Watanzania, hadi sasa tumefanikiwa kukusanya kiasi cha fedha kuweza kuwalipia viongozi wetu watatu, tumemlipia Mhe. Halima Mdee, Mhe. Ester Amos Bulaya na Mhe. Matiko Esther, tayari tumeshalipa pesa hizo,” Kaimu Mwenyekiti Chadema, Said Issa Mohammed.

 

Viongozi wanane wa Chadema pamoja na aliyekuwa Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk Vincent Mashinji jana Jumanne Machi 10, 2020 walihukumiwa kulipa faini ya Sh 350 milioni au kwenda jela miezi mitano baada ya kutiwa hatiani kwa makosa 12 kati ya 13 yaliyokuwa yanawakabili na tayari Mashinji ameshaachiwa huru baada ya Chama Cha Mapinduzi CCM kumlipia faini ya Tsh milioni 30 leo.

Leave a Comment