×

Exim Bank Yatangaza Washindi Droo ya Kwanza ya ‘Chanja Kijanja’

Maofisa waandamizi wa Benki ya Exim Tanzania ambao ni Meneja Mwandamizi Huduma kwa wateja wa Benki hiyo Bw. Frank Matoro (Kushoto), Meneja Masoko, Bi Mariam Mwapinga (Kulia) pamoja Afisa Bidhaaza Rejareja wa benki hiyo Bw Callist Butinga wakionyesha mbele ya waandishi kadi za Mastercard zinazotumiwa nawateja wa benki hiyo wakati wa hafla ya kuwatangaza washindi washindi watano wamwezi waliojishindia simu janja (smartphone) katika kampeni ya ‘Chanja Kijanjana Exim Mastercard’.

Dar esSalaam: Machi 12th, 2020: Benki ya Exim Tanzania hii leo imetangaza washindi watano wamwezi katika kampeni yake ya ‘ChanjaKijanja na Exim Mastercard’. Kampeni hiyo inalenga kuhamasisha wateja wabenki ya Exim kutumia kadi zao za Mastercard katika manunuzi ya mtandaoni aukufanya malipo kupitia mashine za malipo (POS) katika maduka mbalimbali namaeneo mengine nchini.

 

Akizungumza kwenye hafla fupi ya kuwatangaza washindi wa droo ya kwanza  wa kampeni hiyo iliyofanyika Makao Makuu ya benki hiyo jijiniDar es Salaam, Meneja Mwandamizi Huduma kwa wateja benki ya Exim Bwana FrankMatoro aliwataja washindi hao kuwa ni pamoja FahimMohamed ( Dar es Salaam),  Baraka RomKimaro (Dar es Salaam),   Hendrick Hopley (Arusha),   Humphrey Henry (Mbeya) na Amani Makungu (Zanzibar) ambao kila mmoja atazawadia simujanja (smartphone).

 

“Ifahamike kwamba mpaka sasa wateja 40wameshajishindia vocha za manunuzi zenye thamani ya sh 50,000 kila mmoja nazinaendelea kutolewa kila wiki.Pia tunatoa zawadi kama  hizi za leo za simu janja kwa washindi watanokila mwezi hadi mwisho wa mwezi Aprili, 2020 kwani ndio tutakuwa tunafikakilele cha kampeni yetu’’

Meneja Masoko wa Benki ya Exim, Bi Mariam Mwapinga (kulia) akizungumza na waandishi Habari (hawapo pichani) wakati wahafla ya kuwatangaza washindi washindi watano wa mwezi waliojishindia simujanja (smartphone) katika kampeni ya ‘Chanja Kijanja na Exim Mastercard’. Wengine nipamoja na Meneja Mwandamizi Huduma kwa wateja wa Benki hiyo Bw. Frank Matoro(Katikati) pamoja na Mkuu wa Idara ya Muazo ya Kidigitali  Bw Paritosh Babla.

 

‘’Katika kuhitimisha kampeni hii tutatoa zawadikubwa zaidi kwa washindi watatu ambapo mshindi wa kwanza ataenda Dubai, mshindiwa pili ataenda Cape Town, Afrika Kusini na wa tatu ataenda visiwa vya Zanzibar.Washindi hao pamoja na wenza wao watagharamiwa gharama zote ikiwemo Visa,Tiketi ya Ndege pamoja na pesa za matumizi.” alifafanua

 

Kwa mujibu wa Bw. Matoro, Kampeni hiyo inayoendeleaikishirikiana na Mastercard imeanza katikati ya mwezi Februari, 2020 ipo wazikwa wateja wote wanaomiliki kadi za Exim Bank MasterCard, pamoja na wateja woteambao wameomba au wataomba kadi mpya katika kipindi cha kampeni.

 

”Wanachotakiwa wateja wetu ni kufanya miamalayao kupitia kadi ya Exim Bank MasterCard mara nyingi iwezekanavyo kwa kuwa kilamuamala unaongeza nafasi moja ya kushinda.”

 

”Habari njema ni kwamba wateja wanaotumia kadizetu wamekuwa wakifurahia urahisi wanapofanya manunuzi au malipo  ya mahitaji yao kwenye maduka tofauti tofauti(Shopping),ununuzi wa bidhaa  kupitia mtandaoni,malipo wakati wa safari, malipo ya hoteli na shughuli za kitalii.” alisema.

Leave a Comment