VILABU vya England(Uingereza) aya Aston Villa na Brighton & Hove Albion FC vimechangia zaidi ya milo 1,300 ikiwa misaada kwa atu wasio na makazi baada ya mechi za wiki hii kuahirishwa.
Jana, Ijumaa, Ligi Kuu ya England imesitishwa hadi Aprili 3 mwaka huu, kutokana na kuenea kwa virusi vya Corona. Vyakula hivyo vilivyokuwa vimeandaliwa kuuzwa kwa mashabiki, vimetolewa kama msaada kwa wasio na makazi na wenye uhitaji. Hii ni katika kuhakikisha kuwa hakitaharibika.
Klabu ya Brighton Albion pia imejitolea kuwalipa wafanyakazi ambao hawawezi kufika kazini kwa sababu ya hofu ya ugonjwa wa Corona, na wafanyikazi wa kawaida zaidi ya 600 ambao wanafanya kazi kwenye klabu siku ya mechi.
