×

Global Habari Machi 15: Wafuasi 27 Chadema Washikiliwa Na Jeshi La Polisi -Video

Jeshi la Polisi Kanda maalumu Dar es Salaam limeonya na kuahidi kuchukua hatua za kisheria dhidi ya baadhi ya viongozi wa Chadema akiwemo Mbunge wa Kawe Halima Mdee, Esta Bulaya na Meya wa Ubungo Boniphace Jacob walioambatana na wafuasi wa chama hicho kufanya vurugu kwenye eneo la gereza la Segerea wakati mwenyekiti wa chama hicho akitoka gerezani.

 

Kauli hiyo imetolewa hii leo na Kamanda wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam,Lazaro Mambosasa wakati akizungumza na waandishi wa habari juu ya tukio hili ambalo limetokea siku ya March 13 jijini Dar es Salaam ambapo jumla ya watu 27 wanashikiliwa na jeshi la polisi kuhusika na vurugu hizo.

Leave a Comment