Mkutano Mkuu wa Chama cha ACT Wazalendo, umemchagua Maalim Seif Sharif hamad, kuwa Mwenyekiti wa Chama Taifa kwa kura 337, huku washindani wake wa pili akipata kura 20 na mwingine akipata kura 4.
Uchaguzi huo umefanyika usiku wa kuamkia leo Machi 15, 2020, katika mkutano mkuu wa pili wa chama hicho.
Aidha Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Chama hicho, wamemchagua Zitto Kabwe kuendelea na nafasi yake ya Kiongozi Mkuu wa chama kwa kura 276 sawa na asilimia 73.6, huku mshindani wake Ismail Jussa akipata kura 92 sawa na asilimia 24.2, ambapo kura nane zimekataliwa.
Aidha uchaguzi huo unaendeleo leo kwa ajili ya kuwapata, Makamu Mwenyekiti Bara pamoja na Makamu Mwenyekiti Zanzibar.

