×

Mchakato Aussems Kurudi Simba Uko Hivi

KOCHA wa zamani wa Simba, Patrick Aussems, ameweka wazi kuwa hawezi kurejea kuifundisha timu hiyo katika hali yoyote ili kuhakikisha changamoto alizokutana nazo akiwa katika timu hiyo zibaki kuwa sehemu ya historia ya maisha yake kwani sasa ana mipango mingi ya kazi mpya.

 

Aussems ametoa kauli hiyo ikiwa mkataba wa kocha wa sasa wa Simba, Sven Vandenbroeck ukielekea ukingoni kwani alisaini miezi sita na sasa Wanamsimbazi hao wamebakiza mechi 10 kumaliza ligi.

Aidha hivi karibuni mashabiki wa Simba walivamia kwenye ukurasa wake wa Instagram na kumtaka arejee kuifundisha timu hiyo baada ya kufugwa na JKT Tanzania.

 

Akizungumza na Championi Jumamosi, Aussems alisema kuwa, kwa sasa yupo Afrika akikamilisha mazungumzo ya kujiunga na moja ya klabu kubwa lakini hawazi kurejea Simba kwa kuwa itabaki kama sehemu ya historia ya maisha yake ya soka aliyopita kutokana na changamoto alizoziona.

 

“Huu si wakati mzuri wa kusema nakamilisha jambo sehemu gani lakini nipo Afrika kwa ajili ya kitu kikubwa katika sehemu kubwa, nadhani ni wakati wa kusubiria nini kitatokea kwa kuwa bado nina mipango mingi lakini siyo ya kuweza kurudi Simba, hilo haliwezi kutokea kabisa.

 

“Kiukweli siwezi kurejea Simba, tayari nina mipango yangu ya kazi mpya, sitaki kuona narudia changamoto nilizopitia Simba hilo siwezi kuruhusu kabisa kutokea, Simba itabaki kuwa sehemu niliyopita katika maisha yangu ya soka, nimeacha alama nzuri pale na maisha lazima yaendelee,” alisema Aussems.

Leave a Comment