×

Arusha: Hoteli Aliyofikia Mgonjwa wa Corona Yafungwa, Hakuna Kutoka Ndani

MKUU wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo amesema kwamba ndani ya mkoa huo umebainika kuwa na mgonjwa mmoja wa Corona na kwamba hoteli ambayo amekutwa mgonjwa huyo imefungwa na hivyo hakuna anayeingia wala anayetoka.

 

Akizungumza Machi 16 mwaka 2020, Gambo amesema kwa mujibu wa Waziri wa Afya ,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu,  ni kweli wamepata mgonjwa mmoja wa Corona na kwamba juzi  Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) kwa  ndege ya Rwanda Air.

 

Amesema kuwa mgonjwa huyo alifikia kwenye hoteli inayofahamika kwa jina la Temi Valley Hotel ya jijini Arusha na kwamba baadaye alienda Hospitali ya Mount Meru kwa ajili ya kuchukuliwa sampuli na kisha kupelekwa Dar es Salaam ambako kuna maabara ya kupima sampuli za Corona na kubainika ni kweli ana Corona.

 

“Na tulichokifanya sisi kama serikali za ngazi ya mkoa,  kwanza ile hoteli ambayo mgonjwa alifikia tumeifungia na hakuna mtu kuingia wala kutoka kati ya wafanyakazi na wahusika wote waliokuwa wanakaa kwenye hoteli hiyo.  Hatua ambayo tumechukua ni kuchukua sampuli ya uchunguzi kwa watu wote katika hoteli hiyo kubaini kama kuna wengine walioambukizwa.

 

” Lakini hatua ya tatu ambayo tumechukua kama mkoa ni kutenga eneo maalum iwapo atapatikana mgonjwa yeyote ambaye atapelekwa kwenye eneo hilo kwa ajili ya hatua nyingine za matibabu.  Pia tunamfuatilia dereva tksi ambaye alimpakia mgonjwa wa Corona pamoja na familia yake ili naye achunguzwe kama hajapata maambukizi,” amesema Gambo.

 

Amewatoa hofu wananchi wa Mkoa wa Arusha kamba waendelee kuwa watulivu kwani serikali imechukua hatua stahiki katika kukabiliana na ugonjwa huo.  Alileza ambavyo wamefuatilia mtandao wote wa watu ambao kwa namna moja au nyingine walimpokea mgonjwa huyo wanapatikane na kisha kupimwa, lengo ni kuhakikisha maambukizi hayasambai katika mkoa huo .

 

Leave a Comment