×

Trump Ajibizana Vikali Na Meya Kuhusu Janga La Moto Kwa Staili Ya Magufuli

Rais Donald Trump, usiku wa kuamkia leo Jumamosi, Januari 25, aliingia kwenye mjadala mkali na Meya wa Los Angeles, Bi. Karen Bass, kuhusu juhudi za jiji hilo za kurejesha miundombinu na kuruhusu watu kuanza ujenzi wa nyumba zao baada ya janga la moto wa nyika.
Trump alimshinikiza Meya Bass kuwaruhusu watu waanze kurejea mara moja, akionyesha mtindo wa kuwabana viongozi papo kwa papo, kama ule wa Hayati Rais John Magufuli.

Tukio hili lilitokea katika mkutano wa pamoja na waandishi wa habari jana Ijumaa usiku, Januari 24, ambapo Trump alisema kuwa alisikia tetesi kutoka kwa makundi kadhaa kwamba waliambiwa hawataweza kuanza kujenga upya nyumba zao kwa kipindi cha miezi 18.
“Hapana, hapana,” Bass alijibu mara moja. “Hilo si kweli, unaweza kunihakiki kuhusu hilo.”
Trump akajibu: “Watu wanapaswa kuanza leo usiku.”

GOODLUCK GOZBERT KUCHOMA GARI la NABII MKUU -MCHUNGAJI MASHIMO AFICHUA SIRI NZITO JUU ya MADHABAHU..

Leave a Comment