×

Kucha za Amber Rutty Noma

KUCHA za msanii wa muziki wa Bongo Fleva, Mascat Aboubakary ‘Amber Rutty’ zimewaacha watu midomo wazi kutokana na muonekano wake.

 

Amber Rutty aliweka picha akiwa amebandika kucha za bandia kwenye ukurasa wake wa Instagram ambapo watu walishangazwa na muonekano wake kwani ni ndefu sana zilizowafanya wengine kudai amekuwa kama kunguru.

 

“Hizi kucha unaweza kukaa na mpenzi wako mezani akaanza kukupiga mkono akijua kunguru kawavamia, hahahaa,” aliandika shabiki mmoja anayejiita Stella kwenye mtandao huo wa Instagram.

 

Leave a Comment