×

‘Chomoka na Gari Mpya’ ya Championi, Spoti Xtra Yatikisa Mwanza

AMA kweli wanasema hayawi hayawi sasa yamekuwa!  Ile  promosheni namba moja kwa sasa hapa Tanzania  ya bahati nasibu ya Chomoka na Gari mpya aina ya Totoya FunCarge inayoendeshwa na magazeti  bora ya michezo , Championi na SpotXtra tayari imezinduliwa jijini Mwanza.

Timu ya masoko Kanda ya Ziwa  ikiongozwa na afisa wake Khamis Kikasi juzi Jumatatu  ilitinga jijini Mwanza kuzindua  rasmi Chomoka na Gari Mpya  na kushangazwa na mapokeo  makubwa ya promosheni hiyo  kutokana na wasomaji wa magazeti  ya michezo  nchini kujitokeza kwa wingi ambapo wengi wao walichangamkia magazeti yaliyokuwa yakiuzwa huku mamia wakijaza kuponi maalumu kwa ajili ya kutaka kujishindia gari mpya.

Timu ya masoko ilitembelea maeneo mbalimbali ya Jiji la Mwanza ikiwemo, Pasiansi, Kona ya Bwiru,  Igoma, Mecco, Buzuruga, Mabatini, Mwanza mjini , Mkuyuni, Nyegezi Kona, Nyegezi Stand, Mkolani  na mji unaokuwa  kwa kasi wa Buhongwa ambapo baada ya promosheni hii kabambe kuingia katika mji huo watu walitanda barabarani wakionekana kufuatilia kwa umakini promosheni hiyo.

Wasomaji wa magaeti hayo waliya changamkia  na kujaza kuponi zilizowawezesha kuingia kwenye kinyang’anyiro  cha kushinda Gari Mpya  huku wakiahidi kununua magazeti hayo zaidi na zaidi  ili waweze kushiriki bahati nasihu hiyo kikamilifu  na waweze kupata bahati ya kujishindia ndinga hiyo mpya.

 

Hii ni wiki ya nne tangu kampuni ya Global Publishers  ilipozindua  bahati nasibu hiyo kupitia magazeti ya Championi na Spoti Xtra ambapo wasomaji watakaonunua magazeti hayo kwa wingi wataweza kunufaika na  ushindi wa gari mpya aina ya Toyota FunCargo.  Mbali nna zawadi hiyo,  kila  washindi 10 wataondoka na Simu Janja mpya  za mikononi  aina ya  Smart Kitochi zikiwa zimesheheni bando la bure na App ya Global ambayo ndani ina +255 Global Radio  na TV Online.

JINSI YA KUSHIRIKI

Nunua gazeti la Championi na Spoti Xtra kisha fungua ukurasa wa pili ambapo utakutana na  kuponi yenye maelekezo ya kushiriki bahati nasibu  hiyo kwa kujaza kuponi kama maelekezo yalivyo.

JINSI YA KUTUMA

Mpe kuponi muuza magazeti aliye karibu yako au peleka kwenye ofisi za Global Publishers  zilizopo Sinza-Mori Dar es Salaam au tuma kwa njia ya barua  kwa Jishindie Gari, Global Publishers S.L.P 7534 Dar es Salaam.  Kwa maelekezo zaidi piga simu namba 0717020792 au 0672324759.

MASHARTI YA USHIRIKI

Wafanyakazi wa kampuni ya Global Publishers  & General Enterprices Ltd na watoto wa umri chini ya miaka 18 hawaruhusisi kushiriki bahati nasibu  hii.  Kuponi zitumwe kutoka nakala halisi, vivuli (fotokopi) haviruhusiwi.  Mtu anaruhusiwa kutuma kuponi nyingi kadri  awezavyo ili ajiongezee nafasi ya kushinda. Kuponi zote zitachezeshwa kwenye droo ya awamu ya kwanza, ya pili na ya tatu.

Na Johnson James, Mwanza

Leave a Comment