“CCM ni taasisi kubwa, matukio makubwa ya ujenzi wa chama ya nje na ndani ya jamii, maelekezo shughuli zote za CCM zenye asili ya mikusanyiko mikubwa, iwe ya ndani au ya hadhara. Shughuli hizo zisitishwe mara moja kuanzia leo, ili kuunga mkono jitihada za serikali za kupambana na Ugonjwa wa Corona.
“Freeman Mbowe anahamasisha watu kufanya mikutano ya hadhara hapa, Watanzania mpime nani anawapenda, nani anataka kuwatumia. Corona inauwa kweli na ukiipata ni rahisi kuambukiza wengine na eneo rahisi kuambukizana ni kwenye mikusanyiko.
“Hatutaki kufanya siasa katikati ya hatari inayolikabili taifa, lakini kwa sababu bwana Mbowe maslahi yake si hayo, ndio sasa yeye anaelekeza watu waendelee kufanya mikutano, wathamini uhai wao kwanza kabla yakutekeleza maelekezo ya Mwenyekiti wao bwana Mbowe,” Humphrey Polepole, Katibu Itikadi CCM.
