×

Kisa Corona, DC Sabaya: Tutafunga Bar, Supermarket Zote – Video

WAKATI kisa cha kwanza cha mgonjwa mwenye virusi vya Corona kikiripotiwa rasmi nchini Tanzania, juhudi mbalimbali zimeanza kuchukuliwa na serikali wilayani Hai ulipo uwanja wa Kimataifa wa Ndege wa Kilimajaro (KIA) kwa kuzuia mikusanyiko yote, kutoa elimu pamoja na kutenga kiasi cha Tsh milioni 35 kwa ajili ya kujikinga na maambukizi ya ugonjwa huo.

 

Akizungumza kwenye kikao kilichokutanisha wadau wa afya, viongozi wa dini, na watendaji wa kata na tarafa, Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya, amesema wilaya yake ndiyo lango kuu la wageni kutoka katika maeneo mbalimbali duniani kupitia uwanja wa kimataifa wa KIA,  hivyo imeweka mipango mbalimbali kwa ajili ya kukabiliana na kusambaa kwa ugonjwa huo.

 

Mganga Mkuu wa Wilaya ya Hai, Dr Irene Haule, amesema  wameanza kutoa elimu kwa wananchi kuhusu jinsi ya kujikinga na ugonjwa wa Corona huku wakikabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo ya vifaa-tiba vinavyogharimu Tsh milioni 36.

 

Dr Haule amesema kuwa wilaya hiyo tayari imekwishatenga zahanati ya Bomang’ombe kwa ajili ya kuwahuduimia wagonjwa watakaobainika kuwa na ugonjwa wa virusi vya Corona.

 

Mapema jana  Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu, alithibitishwa kuwepo kwa mgonjwa mwenye virusi vya Corona aliyeingia nchini KIA akitokea  Ubelgiji.

 

Leave a Comment