×

#BREAKING: Wagonjwa wa Corona Nchini Wafikia Watatu – Waziri Mkuu

 

WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa ametangaza kuwepo wagonjwa wengine wawili wa virusi vya Corona nchini Tanzania, ambao mmoja ni raia wa Marekani aliyepo jijini Dar es Salaam na raia wa Ujerumani aliyepo visiwani Zanzibar na kufanya jumla ya waathirika wa virusi hivyo nchini wamefikia watatu.

 

“Tayari wagonjwa wawili wamepatikana wa maambukizi ya virusi vya Corona, mmoja kutoka Zanzibar, sampuli zake zililetwa maabara kuu yeye ni Mjerumani (24), yuko kwenye uangalizi, hapa Dar es Salaam tuna Mmarekani (61), na tutaendelea kuwahifadhi hawa hadi tukapojiridhisha tatizo limekwisha basi tutaweza kuwaondoa.

 

“Shughuli za masoko na maduka zitaendelea kama kawaida ila tunaomba msisitizo zaidi kuwasihi wananchi kuepuka mikusanyiko isiyokuwa ya lazima. Vyombo vya usafirishaji tunawasihi watu kuwa ‘level seat’ na kupunguza misongamano.
“Wizara ya Afya ihakikishe vifaa vya kinga ikiwemo vimiminika vya kudhibiti maambukizi (hand sanitizer) vinapatikana katika maduka yote husika kwa bei ya kawaida, Serikali itachukua hatua kali kwa wafanyabiashara wanaopandisha bei,”  amesema Majaliwa.

 

Pia, amesitisha masomo kwa vyuo vikuu na vya kati nchini kuanzia leo March 18, 2020 ili kukabiliana na Virusi vya Corona.

 

Leave a Comment