WAKAZI wa Mkoa wa Dar es Salaam na Watanzania kwa jumla wameombwa kutulia majumbani mwao baada ya shughuli zao za kila siku ili kukwepa maambukizi ya homa ya virusi vya Corona – Covid-19.
Wito huo umetolewa na mkuu wa mkoa huo, Paul Makonda, leo Machi 20, 2020, alipofanya ziara ya kushtukiza katika viwanda, mashirika na taasisi mbalimbali mkoani humo kukagua kama maagizo ya serikali ya kuwataka kujikinga na ugonjwa hatari wa Corona yanafuatwa.
“Wanaopenda kucheza muziki, kwenda club kama leo Ijumaa wachukue tahadhari ya kujikinga dhidi ya Corona. Fungua muziki nyumbani, cheza na familia yako, na wanaoenda baa kunywa, agiza kinywaji unywee nyumbani. Ukikuta basi la mwendokasi limejaa shuka, uoga ni akili; usijifanye jasiri ikaku-cost,” amesema.