Dodoma: Kauli ya Jeshi la Polisi Kuhusu Kumkamata Zitto Kabwe Bungeni - Global Publishers
Imewekwa na on February 8th, 2017 , 10:42:26am

Dodoma: Kauli ya Jeshi la Polisi Kuhusu Kumkamata Zitto Kabwe Bungeni

DODOMA: Mbunge wa Kigoma Mjini na Kiongozi wa Chama cha ACT- Wazalendo, Zitto Zuberi Kabwe jana alijificha ndani ya ukumbi wa bunge mjini Dodoma  kwa hofu ya kukamatwa na Jeshi la Polisi mara tu atakapotoka nje ya ukumbi huo.
Zitto Kabwe kupitia ukurasa wake wa Twitter aliandika  kuwa Polisi wa bunge wamemwambia kuwa watamkakata kwa kosa la uchochezi ambalo yeye mwenye hafahamu ni lipi.
Akizungumzia taarifa hizo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Lazaro Mambosasa  amesema si kweli kwamba Polisi walikuwa Bungeni kumsubiri Zitto atoke wamkamate.
 “Hiyo taarifa yeye mwenyewe ndio anajitangazaia akamatwe lakini sisi hatumkamati kwasababu hatuna ishu nae
 
“Unajua watu wanafikia mahali wanatafuta umaarufu wakamatwe ili wapige mayowe… hatuna mpango wowote wa kumkamata kwasababu hajatenda kosa la jinai”  Amesema Kamanda Mambosasa.

Save

Tupia Comment Yako, Matusi Hapana

Stori zinazo husiana na ulizosoma