DAR: Mwigizaji wa kiume wa Bongo Movies, Kulwa Kikumba ‘Dude’ ametoa nasaha kuwa watu wamrudie mwenyezi Mungu maana muda wowote atarudi kuchukua walio wake.
Akizungumza na Gazeti la IJUMAA, Dude amesema watu wanatembea na vifo mkononi maana kifo hakina hodi, kinaweza kukuchukua muda wowote hivyo ni vyema kutenda yaliyo mema mbele za Mungu hasa katika kipindi hiki kigumu.
“Watu tumrudie Mungu na kutenda yaliyo mema mbele zake, kuishi vizuri na watu maana tuko katika kipindi kigumu na tunatembea na kifo hivyo ni vyema kujiweka safi muda wote,’’ alisema Dude ambaye hivi karibuni amepita pigo la kumpoteza rafiki yake, mwigizaji Mbaraka Ghafool ‘Baki Boban’.
Stori: HAPPYNESS MASUNGA, Ijumaa
