×

Kisa Mo, Orlando Yapandisha Bei ya Mzambia

Orlando Pirates ya Afrika Kusini ni kama wameichungulia Simba, kisha wakagundua kuwa timu hiyo ina fedha nyingi, hiyo ni kutokana kufahamu kuwa timu hiyo kwa sasa ipo chini ya bilionea namba moja kwa vijana barani Afrika, Mo Dewji, kasha ikaona iongeze thamani ya straika wao Justin Shonga ambaye Simba wanamhitaji.

 

Awali timu hiyo ilikuwa ikihitaji kiasi cha shilingi milioni 800 za Kitanzania kwa mchezaji huyo lakini baada ya kuchungulia utajiri wa mwekezaji huyo ndani ya Simba, kila kitu kimeenda tofauti na ilivyokuwa awali kwani thamani ya mchezaji huyo imepanda ghafla.

 

Kwa mujibu wa mtandao wa Transfer Market unaodili na wachezaji, Justine Shonga sasa anamilikiwa na moja ya kampuni kubwa inayaopatikana nchini Arika kusini inayotambulika kama ‘P Management’ ambayo inamiliki wachezaji na makocha wakubwa wanaopatikana barani Afrika.

 

Kampuni hiyo inamiliki wachezaji wakubwa kama Ronald Kampamba wa Nkana FC, Jesse Were wa Zesco FC, Thembinkosi Lorch wa

Orlando Pirates,Tercios Malepe wa Chipa United ,Tshidiso Patjie wa Baroka FC na wengine wengi.

 

Aidha katika wachezaji ambao kampuni ya P Management inawamiliki, Justin Shonga anashika nafasi ya pili kwa kuwa na thamani kubwa nyuma ya Thembinkosi Lorch anayewaongoza wachezaji wote kutokana na kuwa na thamani ya bilioni 2 na nusu huku Shonga yeye thamani yake ikiongezeka kutoka milioni 800 hadi kuwa Sh bilioni moja na milioni 800.

 

Orlando Pirates walimnunua Shonga mwaka 2017 kwa kiasi cha euro 175,000 sawa shilingi milioni 430.3 za Kitanzania, na baada ya kupandisha thamani ya mchezaji huyo kwa sasa na kufikia thamani ya euro 750,000 sawa na Sh bilioni moja na milioni 800.

 

Mpaka kufikia Juni 26, mwaka huu thamani ya mchezaji huyo itapanda hadi kufikia Sh bilioni mbili (euro 850,000) kama ataongeza mkataba mpya wa kuitumikia klabu hiyo kutokana na mkataba aliousaini 2017 wa miaka mitatu unaotarajiwa kumalizika Juni, mwaka huu.

 

Marco Mzumbe, Dar es Salaam

Leave a Comment