WAZIRI Mkuu wa Uingereza, Boris Johnson, ametoa amri ya kuwataka watu wabakie majumbani na kuwapiga faini kwa wale watakaokiuka maagizo hayo.
Katika hotuba yake Johnson amewaambia raia wa Uingereza kwamba lazima wabakie majumbani na iwapo hawatafuata maagizo hayo, polisi watawakamata na kulazimika kuoa faini baada ya kukamatwa.
Sambamba na hilo mikusanyiko ya zaidi ya watu wawili imepigwa marufuku nchini humo. Johnson ameamrisha watakaotoka nje ya makazi yao wawe na sababu maalum.
